Bale atangaza kustaafu soka

Bale atangaza kustaafu soka

Gareth Frank Bale ambaye ni mchezaji anayecheza kama winga katika klabu ya Real Madrid na timu ya taifa ya Wales, ametangaza kustaafu rasmi soka baada ya kudumu kwa miaka 17.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, amethibitisha taarifa hizo huku akisema kuwa anajiona mwenye bahati kubwa kuisha katika ndoto zake kwa kucheza mchezo huo.

“Baada ya kufikiria kwa umakini, ninatangaza kustaafu kwenye klabu na kimataifa, ninawashukuru mashabiki wangu wote,” ameandika Nahodha wa Timu ya Taifa ya  Wales.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags