Baharia wa vita vya pili vya dunia atimiza miaka 100

Baharia wa vita vya pili vya dunia atimiza miaka 100

Baharia wa Wanamaji wa Kifalme Morrell Murphy ambaye aliripotiwa kufariki wakati wa vita vya pili vya dunia amesherehekea siku yake ya kuzaliwa ambapo ametimiza miaka 100.

Mwamba huyo wa bahari kutoka Lisburn, alikuwa kwenye meli ya HMS Capel wakati ilipoharibiwa na manowari ya Ujerumani mnamo mwaka 1944, siku nne baada ya shambulio hilo familia yake ilifahamishwa kuwa Murphy alikuwa ameuawa.

Familia hiyo ilipokea barua ya salamu za rambirambi kutoka kwa Mfalme George wa Sita lakini muda mfupi baadaye Morrell alipatikana akiwa hai na mwenye afya katika nyumba ya familia.

Morrel kwasasa anaishi County Down na mjukuu wake Jennifer aliandaa karamu ya kuadhimisha miaka 100 ya kuzaliwa kwake.

"Ni vigumu kuamini kwamba sasa nina umri wa miaka 100. Ni vigumu kuamini kwamba nimeishi miaka hii yote lakini bado ninafurahia maisha,” amesema Morrel.

Alijiunga na Jeshi la Wanamaji la Kifalme akiwa na umri wa miaka 19, vita vya pili vya dunia vilipokuwa vikiendelea.

Mnamo mwezi Disemba mwaka 1944, alinusurika shambulio la Wajerumani katika idhaa ya Kiingereza ambayo iliua zaidi ya washiriki wenzake 70 kwenye HMS Capel.

Aliokolewa na jeshi la wanamaji la Marekani na kupelekwa Ufaransa. Hivyo hii ilimaanisha kuwa mamlaka ya Uingereza haikujua kuwa bado yupo hai.

Chanzo BBC






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post