Babu Tale, Amjibu P Funk Majani

Babu Tale, Amjibu P Funk Majani

Aloooooh! Mnasema nihame bongo niende wapi mie ahahha! Basi bwana siku chache baada ya yule Baba wa binti maarufu Paula kajala, bwana P Funk Majani kumwaga povu kuhusu Lebo ya Muziki ya WCB kunyonya wasanii wake, sasa Meneja wa msanii Diamond , Babu Tale akatoa ya moyoni na kumpa majibu yanayo mstairi.

Babu Tale alifunguka hayo kupitia mahojiano yake na waandishi wa habari na kusema kuwa“Kama mkongwe kasema si vizuri kubishana naye acha aseme namuheshimu sana P Funk, Mikataba ya WCB haipo kwenye maiki ama kamera. Ulishawahi kumuona mtu amebandika mikataba kwenye kamera au maiki? Heshima ya Majani kwenye hii industry ya muziki ni kubwa, basi tumwache aseme atakacho jiskia” amesema Babu Tale

Aidha Meneja wa Mondi bwana aliendelea kumwaga povu“La ndani linabakia ndani, ukimwona mtu analitoa la ndani kuwa la nje hajafundwa huyo. Nina miaka mingi kwenye industry ya muziki, nazungumza ninachoikifahamu, lakini tunabadilisha kutoka kwenye muziki wa kawaida kuwa biashara.

"Lazima kuwe na mikataba na makubalianao na makubaliano ni ya ndani, unapoona mtu anasimama kuyachambua makubalianao, ana mashaka. Na ukiona mtu anachambua mkataba wa pande mbili ambao hahusiki kwa namna yoyote achana naye, muheshimu. Amesema Babu Tale

Mmmmmh! Mbona mazito haya wanangu wa Mwananchi Scoop je mnakubaliana na P Funk Majani, dondosha komenti yako hapo chini mtu wangu wa nguvu


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post