Baba mzazi wa AKA afunguka

Baba mzazi wa AKA afunguka

Baada ya washukiwa wa mauaji ya mwanamuziki kutoka Afrika Kusini, AKA kukamatwa na kufikishwa katika Mahakamani ya Hakimu Mkazi jiji Durban siku ya jana Februari 29, baba mzazi wa AKA, Tony Forbes amefunguka na kueleza kuwa hisia zake zinamwambia muhusika mkuu bado hajakamatwa.

Tony ameyasema hayo kufuatiwa na mahojiano yake na waandishi wa habari wakati alipokuwa akitoka Mahakamani ambapo alieleza kuwa anaamini muandaaji mkuu aliyekuwa nyuma ya mauaji hayo bado hajakamatwa na anaamini ndiye mshitakiwa wa kwanza kwenye kesi hii.

Washukiwa waliopelekwa Mahakamani siku ya jana walikuwa Siyanda Myeza (21), Lindokuhle Ndimande (29), Lindani Ndimande (35), ambao ni mtu na kaka yake, Lindokuhle Thabani (30) na Mziwethemba Myeza (36).

Hata hivyo kesi hiyo siku ya jana ilihairishwa mpaka Machi 6, 2024, na endapo washukiwa hao wakitaka dhamana maombi hayo yanaweza kusikilizwa kuanzia Machi 14.

Ikumbukwe #AKA (35), aliuawa kwa kupigwa risasi Februari 10, mwaka jana, alipokuwa akitembea na rafiki yake nje ya mgahawa #Durban, Afrika Kusini.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags