Baba Burna Boy aweka wazi anavyojivunia mwanaye

Baba Burna Boy aweka wazi anavyojivunia mwanaye

Baba mzazi wa mwanamuziki wa Nigeria Burna Boy, Samuel Ogulu ameweka wazi jinsi anavyovutiwa na mafanikio ya kijana wake, hii ni baada ya mwanaye kuupiga mwingi katika onesho lilifanyika jijini London.

 Kwa mujibu wa tovuti ya ‘Legit.ng’ Samuel Ogulu alionesha furaha yake kwa kijana wake kwa kueleza kuwa amezaa jembe na anajivunia sana mafanikio ya kijana wake.

 Utakumbuka wikiendi hii Burna Boy aliteka vichwa vya habari baada ya kuujaza uwanja katika show yake aliyoifanya katika uwanja ‘London Stadium’ wenye uwezo wa kuchukua watu 80,000.

 Kufuatia na onesho hilo wadau mbalimbali walitoa maoni yao kwenye mitandao ya kijamii kwa kudai kuwa msanii huyo anaendelea kukua na kubadilika kila uchwao kutokana na kuwepo na mabadiliko kwenye kila show zake.

Aidha baada ya onesho hilo Burna Boy alitoa shukrani kwa mashabiki wote waliofika kwenye tamasha lake lililotikisa jiji zima la London.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags