Baba amfanyia binti yake sherehe baada ya kuachika

Baba amfanyia binti yake sherehe baada ya kuachika

Mwanaume mmoja kutoka nchini India anayefahamika kwa jina la Prem Gupta amfanyia sherehe binti yake baada ya kuachika.


Binti wa Prem, aitwaye Sakshi Gupta aliolewa mwaka 2022 na Sachin Kumar, ndoa yao ilifika ukingoni baada ya mwanadada huyo kutoa taarifa kwa wazazi wake kuhusiana na ukatili na manyanyaso anayoyapata kutoka kwa mumewe na familia ya mwanaume huyo.

Baba mzazi wa binti huyo baada ya kugundua ukatili anaopitia mwanaye akaamua
kumpa ushirikiano ili aweze kupata talaka yake na kuondoka katika nyumba hiyo akiwa salama.

Baada ya mchakato wa talaka kumalizika, baba mzazi wa binti huyo, Prem aliamua kualika watu wakiwa na ngoma, fataki na baruti na kuelekea katika nyumba aliyokuwa akiishi binti yake Sakshi na mumewe kwa ajili ya kumrudisha nyumbani.

Prem baada ya kumchukua binti yake amewataka wazazi wengine wachukue mfano wake kwa kueleza, Amesema kuwa,

“Wakifunga ndoa kunakuwa na sherehe za kufurahi, hivyo, pale upande wa mume na familia ya mume wanapokuwa hawana mwenendo mzuri kitabia na kimatendo, basi ndoa ikishindikana binti arudishwe tena kwa wazazi wake na apokelewe kwa heshima ile ile aliondoka nayo siku ya harusi kwa sababu watoto wa kike ni wenye kuthaminiwa”






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags