Baada ya Takeoff kuuawa, Quavo aanza mapambano dhidi ya unyanyasaji

Baada ya Takeoff kuuawa, Quavo aanza mapambano dhidi ya unyanyasaji

Mwanamuziki Quavo ajitokeza kukutana na watu mashuhuri wa kisiasa akiwemo Kamala Harris siku ya jana kupinga unyanyasaji wa kutumia bunduki.

Quavo amekutana na wanasiasa hao katika Mkutano wa Wabunge wa Baraza la Wawakilishi wa Watu Weusi, Washingtonni kwa lengo la kujadili jinsi ya kupunguza kiwango cha unyanyasaji wa kutumia bunduki, ikiwa ni baada mara baada ya kifo cha mpwa wake TakeOff ambaye alifariki kwa kupigwa risasi mwaka jana.

Kifo cha TakeOff bado kinaendelea kuwa mtihani kwa Quavo kama alivyowahi kueleza kuwa bado anamkumbuka sana marehemu TakeOff anampenda na kuna wakati hupatwa na huzuni hadi kufikia hatua ya kulia kila akimkumbuka.

TakeOff alikuwa ni mmoja ya rapper wa kundi la Migos, lililokuwa na wasanii watatu TakeOff, Quavo na Offset.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags