Baada ya ndoa yake kuvunjika, aanzisha kikundi cha kuruka kamba kupunguza mawazo

Baada ya ndoa yake kuvunjika, aanzisha kikundi cha kuruka kamba kupunguza mawazo

Wakati baadhi ya akina mama nchini wakiendelea kuunda vikundi vya kuwezeshana ambavyo vinafahamika kama vikoba, na vinginevyo vinavyokuwa kwa kasi siku za hivi karibuni.

Jambo hilo limekuwa tofauti kwa mwanamke aitwaye Pamela Robinson kutoka Chicago yeye aliamua kuanzisha kikundi cha kina mama kwa ajili ya kuruka kamba kinachojulikana kwa jina la (Beyond the ropes), chenye zaidi ya wanawake 40 huku dhumuni la kikundi hicho likiwa ni kubadilishana mawazo, kuhusu familia na mambo mengine.

Pamela kupitia video yake alieleza kuhusiana na kilichomsukuma mpaka kuanzisha kikundi hicho kwa kusema kuwa mwaka 2016 msongo wa mawazo ulisababisha aanzishe kikundi baada ya ndoa yake ya miaka 20 kuvunjika, ili kutafuta furaha ndipo akaanzisha kikundi cha kuruka Kamba.

Kwenye video hiyo Pamela alisema,
“Tunapaswa kuanza kuruka kamba kama tulivyokuwa tukizoea huko nyuma utotoni, tunatumia muda mwingi kutunza waume zetu , watoto na wazazi lakini hatuna muda wa kujitunza wenyewe.

Tunafanya zaidi ya kuruka Kamba, tunaimba, tunacheza, tunataniana, kama tulivyofanya kipindi tuko watoto. tunazungumza juu ya kukoma kwa hedhi, mabinti wanaokua kukusanyika na wanawake wengine kujifunza mambo mapya.”

Pamela anadai kuwa wanawake wengi waliojiunga kwenye kundi hilo walikuwa na msongo wa mawazo lakini kutokana na mchezo huo inawasaidia kurudisha furaha.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags