Baada ya kipigo Cassie alienda mtoko na Diddy

Baada ya kipigo Cassie alienda mtoko na Diddy

Baada ya kusambaa kwa video zikimuonesha Diddy akimpiga aliyekuwa mpenzi wake Cassie, huku baadhi ya wadau mbalimbali wakimshamulia rapa hiyo na sasa imeripotiwa kuwa siku mbili baada ya kipigo hicho Cassie alitoka out na Diddy.

Kwa mujibu wa tovuti ya ‘Hollywoodunlocked’ imeeleza kuwa baada ya kipigo wawili hao walimaliza tofauti zao ambapo walioneka tena wakiwa pamoja Machi 7, 2016 katika onesho la 'The Perfect Match, huku Cassie akionekana na michubuko kwenye mkono wa kushoto, paja pamoja na miguu.

Video hiyo ya Diddy ilionesha kwa mara ya kwanza na runinga ya Cnn ambapo ilimuonesha mkali huyo wa Hip-hop akimshambulia mpenzi wake wa zamani Cassie tukio lililotokea Machi 5, 2016 kwenye hoteli ya ‘InterContinental’ amabyo kwasasa imefungiwa kulingana na malalamiko ya Cassie.

Hata hivyo kufuatia na kutolewa maneno machafu katika mitandao ya kijamii Diddy siku ya Jana Mei 19, 2024 kupitia ukurasa wake wa Instagram aliomba radhi kwa kile kilichotokea huku akidai kuwa hakuwa kwenye utimamu wa akili na yuko tayari kwenda kupatiwa msaada wa kisaikolojia ili kuwa mtu mwema.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags