Baada ya Kayumba kudai amekua, Mama yake amtaka aoe

Baada ya Kayumba kudai amekua, Mama yake amtaka aoe

Mwanamuziki Kayumba atuma salamu kwa mama yake kuwa tayari amekuwa mtu mzima.

Kayumba ame-share video ikimuonesha akiwa na mama yake na kuandika, "salamu ziende kwa mama mwanaye nimekuwa" kupitia ujumbe huo mama yake hakukaa kimya naye ali-share video kupitia ukurasa wake wa Instagram kumtaka Kayumba aoe kama amekuwa.

Ujumbe huo aliandika Kayumba kutokana na wimbo wake mpya wa ‘Gentlemen’ ambao umetoka hivi karibuni, na moja katika mistari iliopo kwenye wimbo huo ni ujumbe unaofanana na aliyoandika.

Hii si mara ya kwanza kwa msanii huyo kuimba mistari yenye kumtaja mama yake, kwenye wimbo wa 'mama' uliyotoka miaka mitatu iliyopita pia aliimba na kutoa sifa nyingi na shukrani kwa mama yake.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags