‘Klabu’ ya #AzamFC imefikia makubaliano na akademi ya Yeleen Olympique ya nchini Mali kwa ajili ya kumnunua mchezaji wa kimataifa wa nchi hiyo, Yoro Mamadou Diaby.
Beki huyo ambaye alikuwa kwa mkopo kwenye ‘klabu’ ya Stade Malien de Bamako, atajiunga rasmi na Azam FC kuanzia msimu ujao wa 2024/25.
Akiwa Stade Malien de Bamako, Yoro aliisadia klabu hiyo kufika robo fainali ya Kombe la Shirikisho, akiifungia ‘timu’ yake mabao katika mechi zote mbili za robo fainali dhidi ya Dreams FC ya Ghana.
Yoro amewahi kuzichezea ‘timu’ zote za vijana nchini kwake, kuanzia ile ya chini ya 17, chini ya miaka 20 na chini ya miaka 23.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi
Leave a Reply