Australia kupiga marufuku matumizi ya TikTok

Australia kupiga marufuku matumizi ya TikTok

Serikali kutoka nchini Australia mbioni kupiga marufuku matuminzi ya TikTok katika vifaa vya Serikali na itachukua hatua hiyo kwasababu za kiusalama ikiungana na Marekani, Canada  Newzealand  Ufaransa na Uingereza ambazo pia zipo katika mchakato huo.

Katazo hilo linatokana na onyo lililotolewa na nchi za Magharibi kuhusu mtandao huo wa China wakidai unatumiwa na wahusika kuwapeleleza watumiaji wake.

Hivi karibuni Tiktok imekuwa ikikanusha tuhuma hizo na kudai haijawahi na haitasambaza taarifa za wateja wake kwa Serikali ya China.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post