Aucho afunguka ishu ya tuzo ligi kuu

Aucho afunguka ishu ya tuzo ligi kuu

Kiungo wa Yanga, Khalid Aucho amesema anafurahia maisha ndani ya Yanga kutokana na timu hiyo kumfanikishia malengo yake makubwa kwenye soka ya kutwaa mataji, lakini kwake ishu ya tuzo siyo kubwa sana

Aucho amefunguka hayo siku chache baada ya Kamati ya tuzo za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kufanya uteuzi wa washiriki katika makundi mbalimbali ya tuzo huku jina lake likikosekana.

Akizungumza na Mwanaspoti, Aucho amesema "Tuzo sio kipaumbele huu ni muda wetu sisi kama wachezaji kuzingatia michezo miwili migumu iliyo mbele yetu kuhakikisha tunatwaa taji la Afrika kwa mara ya kwanza tangu michuano hiyo imeanzishwa tukiwa ndani ya timu hii;

"Baada ya orodha ya wachezaji wanaowania tuzo za msimu huu kutoka mambo yamekuwa mengi nimeongea na viongozi kuwaeleza kuwa hilo lisitutoe mchezoni tuzingatie fainali mbili zilizo mbele yetu mimi nimefuata mataji siyo tuzo"

"Nikichukua tuzo ni ya kwangu binafsi timu hakuna inachokiingiza lakini nikiwa miongoni mwa wachezaji watakaoifanya Yanga inatwaa taji la Afrika ni rekodi kubwa itaandikwa vizazi hadi vizazi;

"Kila mchezaji ana malengo yake mimi napenda kuwa mchezaji ambaye anaipa timu yake mafanikio kama kutwaa mataji, kufika hatua kubwa kwenye mashindano hilo nimeweza kulifanikishwa kwa misimu miwili niliyocheza Yanga." alisema kiungo huyo.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post