Auawa na Mumewe

Auawa na Mumewe

 It’s another Monday wanangu wa mwananchiscoop kwenye gumzo mitandaoni kuna taarifa za kusikitisha kidogo ambazo zimewashitua watu wengu kutokana na mwadada  maarufu huko  jijini Mwanza anaejulikana kwa jina la  Swalha, aliyekuwa akijishughulisha na masuala ya urembo yaani  (make-up artist) ameuawa kwa kupigwa na risasi na mumewe usiku wa kumkia  May 29.

Tukio hilo  ambalo limetokea nyumbani kwa wanandoa hao huko Buswelu huku chanzo kikielezwa kuwa ni wivu wa mapenzi, taarifa kutoka kwa watu wa karibu zinasema kuwa mume wa Swalha anayejulikana kwa jina la Said alichukua uamuzi huo kutokana na kile kinachodaiwa kuwa ni wivu wa kimapenzi.

Aidha tatizo kubwa mpaka kufikia mauaji hayo ni kuwa Swalha alienda kuangalia mpira na akachelewa kurejea nyumbani, hivyo basi Mumewe hakufurahishwa na kitendo cha mkewe kuchelewa kurudi nyumbani ndipo  kukazuka ugomvi baina ya wawili hao  hali iliyopelekea mume wa Swalha kumfyatulia risasi.






Comments 1


  • Awesome Image
    Sylvester A Mwitala

    Hasara na hasara,ukiweza kivikilia hasira utajikoa nafsi yako,na mara nyingi hasira huja ghafla na baada ya muda huisha,haia huzaa majuto na kujiuliza sana,utaanza ningejua,au ningeacha,au si ningeondoka tu na mengine mengi. Tudhibiti hasira zetu

Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags