Atumia ndege kama usafiri wa kwenda chuo

Atumia ndege kama usafiri wa kwenda chuo

Mwanafunzi mmoja , aitwaye Tim Chen anayechukua course ya Uchumi katika Chuo Kikuu cha British Columbia (UBC) kilichopo nchini Canada amekuwa akitumia usafiri wa ndege kwenda chuo na kurudi nyumbani anapoishi na wazazi wake Calgary.

Tim kufuatiwa na mahojiano yake aliyoyafanya na kituo cha runinga cha #CTV ameeleza kuwa alifanya uamuzi huo kutokana na kupanda kwa kodi ya pango (chumba) alichokua akiishi ambapo kilikuwa kikigharimu dola 2,500 ikiwa ni zaidi ya tsh 6.3 milioni kwa mwezi.

Kutokana ana bei hiyo kupanda ilimbdi atafute njia nyingine ambayo atakayotumia kufika chuoni hapo, ndipo akaamua kutumia usafiri wa ndege kwende shule na kurudi nyumbani kwao.

Tim alieleza kuwa hakuna ugumu kwake kutumia usafiri huo kutokana na kuwa na vipindi viwili kwa wiki ambapo alidai kuwa anatumia dola 150 katika usafiri wa kwenda na kurudi, ambapo kwa mwezi anatumia dola 1,200 ikiwa ni zaidi ya tsh 3 milioni ambapo asema kuwa ni pesa ndogo kuliko aliyokuwa akitoa kwenye chumba alichopanga.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags