Aslay: mimi siyo dogo

Aslay: mimi siyo dogo

Mwanamuziki Aslay Isihaka amewatolea uvivu wanaodai kuwa sasa hivi hana jipya kwenye muziki kwani hajawahi kutoa ‘kolabo’ na wasanii kutoka nje ya nchi.

Aslay amewatolea maneno wanaomsema ikiwa zimepita siku chache tangu aachie ngoma yake iitwayo #Shu ambayo kwa sasa inaonekana kufanya vizuri kwenye mitandao ya kuuzia muziki, huku mashabiki wengi wakionekana kuupenda wimbo huo kwa kuji-‘rekodi’ video mbalimbali za wimbo huo.

Kupitia ukurasa wake wa #Instagram ame-post video za mashabiki wake zikiwaonesha kupendezwa na hiyo, na kuambatanisha maneno yasemayo,

“Dogo kafeli dogo hana jipya oooh dogo hana ‘kolabo’ za kimataifa sasa nyinyi walimu wa mathe nikitoa hiyo KOLABO nitawauliza hapa ni wapi, halafu sema me sio dogo.”






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags