Askofu Gwajima: klabu ya Simba iombe radhi kuingia na jeneza kwenye simba day

Askofu Gwajima: klabu ya Simba iombe radhi kuingia na jeneza kwenye simba day

Duuuuuh! kumekucha basi bwana siku ya juzi kulizuka gumzo sana katika siku ambayo klabu ya simba iliazimisha miaka 14 ya simba day, gumzo hilo lilitokea baada ya msanii wa bongo fleva Tundaman kuingia na jeneza uwanjani kitendo hicho ambacho baadhi ya watu wa dini na wengine kwa ujumla kuja juu na kutokupendezwa na kitendo hicho.

Askofu Msaidizi wa Jimbo la Katoliki Bukoba, Methodius Kilaini Alilaani kitendo cha Klabu ya Simba kutumia Msalaba na kusema kuwa ni Dharau na kufuru kubwa kwa waumini wakristo.

Kupitia ukurasa wake wa twiter Askofu Gwajima aliandika kuwa “Tukio la Kuingia na Jeneza, Msalaba, na mavazi ya kiongozi wa Imani kwenye sherehe za Simba Day ni mzaha uliopita kiwango. Litakuwa jambo la busara kama Klabu ya Simba itaomba radhi hadharani kwa mashabiki na watu waliochukizwa na Mzaha ule. Mungu Wetu Hadhihakiwi.” Ameandika Askofu Gwajima

Embu dondosha komenti yako hapo chini mtu wangu wa nguvu je ilikuwa ni sahihi simba kufanya vile au la?






Comments 1


  • Awesome Image
    Balikeka Andrea

    Kwakweli Imani si jambo la kuchezea. Imani hubeba mambo mengi ndani yake

Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags