Ashitakiwa kwa kumuua mkewe kisa bili ya hospitali

Ashitakiwa kwa kumuua mkewe kisa bili ya hospitali

Mwanaume mmoja kutoka nchini Marekani aliyefahamika kwa jina la Ronnie Wiggs ameshitakiwa kwa kosa la kumuua mkewe akiwa Hospitali baada ya kushindwa kulipa ‘bili’ ya matibabu ya mkewe.

Kwa mujibu wa tovuti ya The Mirror imeeleza kuwa Ronnie alimkaba mkewe na kumziba mdomo mpaka kushindwa kupata pumzi na kupelekea kifo cha mwanamke huyo akiwa hospitalini hapo.

Hata hivyo baada ya kubanwa na polisi mwanaume huyo alikiri kutenda kosa hilo lakini amejitetea kwa kudai kuwa amemuua mkewe huyo kutokana na kushindwa kumuhudumia mke wake ikiwemo kulipa gharama za Hospitali hiyo ijulikanayo kama ‘The Associated Press’,

Mke wa Ronnie Wiggs alikuwa akiugua kwa muda mrefu ugonjwa ambao haukuwekwa wazi na ilikuwa sio mara ya kwanza kuhudhuria hospalini hapo kwa ajili ya matibabu endelevu.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags