Arsenal, Calafiori ni suala la muda tu

Arsenal, Calafiori ni suala la muda tu

Imeripotiwa kuwa, Arsenal inakaribia kufikia makubaliano ya kumnunua beki wa Italia na Klabu ya Bologna, Riccardo Calafiori.

Aidha inaelezwa kuwa, Bologna imeweka dau la pauni milioni 42 kuwa thamani ya nyota huyo mwenye umri wa miaka 22 ambaye msimu uliopita alikuwa msaada kikosini hapo kumaliza nafasi ya tano kwenye msimamo wa Serie A na kupata tiketi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.

Arsenal wanatarajia kukamilisha usajili wa beki huyo wa kati wiki hii baada ya kufanya mazungumzo zaidi na Calafiori ambaye ameonesha kiwango kizuri kwenye michuano ya Euro 2024 inayofikia tamati kesho Jumapili huko Ujerumani.

Katika michuano ya Euro 2024, Calafiori alikuwa na kikosi cha Italia kilichoishia hatua ya 16 bora.
.
.
.
#MwananchiScoop






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags