Muigizaji mkongwe kutoka nchini Marekani Arnold Schwarzenegger anatarajia kufikishwa mahakamani baada ya kumgonga na gari Mwanamama Joanne Flickinger.
Kwa mujibu wa #TMZ inaeleza kuwa wamekutana na kesi hiyo mpya ambapo mwanamama huyo aliyekuwa akiendesha baskeli kudai kuwa mwezi #Februari mwaka huu aligongwa na #Arnold kwa makusudi kwa sababu muigizaji huyo alikuwa akiendesha gari kwa mwendo kasi.
Aidha kufuatia tukio hilo #Flickinger amedai kuwa lilimsababishia majeraha makubwa kwenye mwili wake, licha ya muigizaji huyo kushuka na kutoa msaada.
Kufuatia tukio hilo muigizaji huyo hajatoa tamko lolote mpaka sasa.

Leave a Reply