Ariana kumlipa Dalton zaidi ya Tsh 3 bilioni

Ariana kumlipa Dalton zaidi ya Tsh 3 bilioni

Baada ya ‘kesi’ kuunguruma mahakamani ya wanandoa Ariana Grande na Dalton Gomez kuhusiana na muafaka wa talaka yao hatimaye wamemalizana huku mrembo huyo akitakiwa kulipa fidia ya pesa za wakili wa Dalton aliyesimamia kesi.

Kwa mujibu wa TMZ inaelezwa kuwa wawili hao kabla ya kuingia katika ndoa ‘walisaini’ na kufanya makubaliano ya umiliki wa vitu ambapo pindi watakapo achana Ariana atatakiwa kumlipa Dalton zaidi ya tsh 3 bilioni.

Kulingana na masharti ya makubaliano hayo Dalton alipokea nusu ya mapato yote ya mauzo ya nyumba yao ya zamani iliyoko Los Angeles.

Ikumbukwe tu wawili hao walifunga ndoa mwaka 2021.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags