Ariana Grande na Gomez wamalizana

Ariana Grande na Gomez wamalizana

Baada ya kutengana mwaka mmoja uliopita huku kesi yao ikirindima miezi sita mahakamani, hatimaye mwanamuziki Ariana Grande na aliyekuwa mumewe Daliton Gomez wamepeana talaka rasmi jana Machi 19, katika mahakama ya juu jijini Los Angeles.

Ariana amekubali kumlipa Gomez dola 1.25 milioni zaidi ya Sh3 bilioni ikiwa ni sehemu ya makubaliano ya kuvunjwa kwa ndoa hiyo.

Malipo hayo yanakuja baada ya wawili hao kuingia mkataba kabla ya ndoa (Prenuptial agreement) unaolazimisha kuwa endapo wakaachana basi Grande atatakiwa kumlipa Gomez kiasi hicho cha pesa pamoja na mgawanyo wa pesa watakapouza nyumba waliyokuwa wakiishi iliyopo Los Angles.

Ikumbukwe kuwa Ariana Grande na Dalton Gomez walifunga ndoa Mei 15, mwaka 2021, huku ndoa yao ikidumu kwa miaka mitatu tu.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags