Arafat Ally: Yanga tunaanza tulipoishia

Arafat Ally: Yanga tunaanza tulipoishia

Aloooooweee! aloooooteeenaa! Basi bwana wakati huku watoto wa msimbazi wanasaini mkataba mnono, huku nako wananchi hawajakaa nyuma bwana kupitia mkutano wao na waandishi wa habari, Makamu wa raisi wa klabu ya Yanga alifunguka na kuwaeleza wananchi kuhusiana na wiki ya wananchi na kueleza kuwa.

"Agosti 6 ndiyo siku pekee ambayo wana Yanga wataona Makombe yote ambayo tumebeba msimu ulioisha kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, pia msimu ujao tutaanza tulipoishia kwa sababu tumefanya sajili bora za kuongeza mafanikio katika kikosi chetu” amesema Arafat Ndiye

Aidha aliendelea kwa kueleza kuhusiana na burusani zitakazo kuwepo katika kilele hicho cha siku ya wananchi “Kila kitu ni Byuti Byuti kuelekea wiki ya Mwananchi kutakuwa na burudani ya kutosha kutoka kwa wasanii mbalimbali pia mtaona vitu byuti uwanjani kutoka kwa wachezaji wetu, Yanga hatuokoti tunasajili ma MVP” amesema Arafat Ndiye






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags