Apple Music Yamtangaza Lamar Kuwa Rapa Bora Wa Mwaka

Apple Music Yamtangaza Lamar Kuwa Rapa Bora Wa Mwaka

Mwanamuziki wa Marekani Kendrick Lamar ametajwa kuwa rapa bora wa mwaka 2024.

Kupitia mtandao wa kuuza muziki ‘Apple Music’ Lamar ametajwa kuwa ndio rapa mwenye ushawishi mkubwa katika mitandao ya kijamii kwa mwaka huu kupitia nyimbo za kurushiana madongo alizokuwa akimjibu rapa Drake.

Mwaka huu pekee, Kendrick amesherehekewa kama mshindi kwenye ngoma za kurushiana maneno (Disstrack) katika historia ya hip-hop huku akipata uteuzi kadhaa kwenye tuzo za Grammy kupitia wimbo wa “Not Like Us”, mbali na hilo pia kupitia mafanikio hayo alipata nafasi ya kutumbuiza kwenye hafla ya Super Bowl mwaka 2025.

Mafanikio hayo yamewafurahisha mashabiki na wadau mbalimbali kwani mwanamuziki huyo amepata mafanikio hayo bila hata kutumia nguvu ya kutoa album huku akitarajia kuachia album mwaka 2025.

Ikumbukwe kuwa bifu la Drake na Lamar lilianza baada ya Lamar kutoa ngoma iitwayo ‘Like That’ akijitambulisha kuwa yeye ni bora kuliko Drake huku akidai kuwa amewazika mastaa wote wanaomsapoti Drake kupitia albumu yake ya ‘For All The Dog’.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags