Apple kuwalipa watumiaji wa iphone za zamani

Apple kuwalipa watumiaji wa iphone za zamani

Kampuni ya Apple inatakiwa kuwalipa watumiaji wa simu za iphone za zamani nchini Canada baada ya watumiaji kushinda kesi ya Batterygate kesi ambayo ilikuwa inaonesha kampuni hiyo ilikuwa ikiharibu Battery ili waweze kuuza betri zilizozopo kwenye stoo yao pamoja na kuuza simu mpya.

Kwa mujibu wa CBC News Apple italipa $14.4 milioni kumaliza kesi hiyo, huku kila mtumiaji ambaye amekumbana na tatizo hilo atalipwa kuanzia dola 17.50 hadi $150.

Ikumbukwe kuwa kesi hiyo ilianza mwaka 2017 ambapo watumiaji walionesha ushahidi wa kampuni hiyo kuharibu battery kwa kutumia iOS, hata hivyo kampuni hiyo iliomba radhi kwa watumiaji wake na kuahiudi kupunguza bei za betri.

Wateja ambao watalipwa ni wale walionunua Iphone za mwaka 2017 ambazo ni iPhone 6, 6 Plus, 6s, 6s Plus, au iPhone SE, 7 au 7 Plus.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags