Apiga magoti masaa 21 kumuomba msamaha ex wake

Apiga magoti masaa 21 kumuomba msamaha ex wake

Mwanaume mmoja kutoka nchini China ambae hakufahamika jina lake, picha  zake zimesambaa mtandaoni zikimuonyesha akiwa amepiga magoti kwenye mvua nje ya ofisi ya ex wake akitaka warudiane.

Mwanaume huyo alitumia masaa 21 akiwa amepiga magoti akiwa na maua njee ya jengo la ofisi ya ex wake huko Dazhou, mjini Sichuani kuanzia saa 1 jioni machi 28 hadi saa 10 siku iliyofuata.

Lengo lake kubwa likiwa kuonana na ex wake ili kumuomba msamaha warudiane, watu waliokua eneo hilo walimsihi kuondoka sababu anajiabisha ila hakua tayari kuaondoka, inasemekana aliondoka asubuhi iliyofuata baada yakutokuonana na x wake huyo.

Afisa wa polisi nchini humo aliviambia vyombo vya habari kuwa “alisema mpenzi wake aliachana naye siku chache zilizopita, anataka kumwomba msamaha na alitumai angeweza kuchumbiana naye tena,” alisema polisi.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags