Antony Joshua: Nikipoteza mpambano huu nastaafu

Antony Joshua: Nikipoteza mpambano huu nastaafu

Antony Joshua, bondia kutoka nchini Uingereza anayetarajia kuzichapa na Jermaine Franklin, Aprili 1, 2023 ndani ya O2 Arena, jijini London ametoa kauli hiyo baada ya kuwa na matokeo mabaya ulingoni kwa muda mrefu.

Bingwa huyo mara mbili wa dunia atapanda ulingoni kutetea heshima yake baada ya kupigwa mara mbili na Oleksandr Usyk, huku pambano lake la mwisho kushinda likiwa Desemba 2020.

Bondia huyo alieleza kuwa, "Hakika nitastaafu kama nitapoteza tena, sipo hapa kushindana na watu, kama watu hawataki nipigane sitopigana, sio suala la pesa, ni ushindani uliopo ndani yangu.” 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags