Anayeshikilia rekodi ya kucha ndefu aeleza changamoto anazo kumbana nazo

Anayeshikilia rekodi ya kucha ndefu aeleza changamoto anazo kumbana nazo

Diana Armstrong ambaye anashikilia rekodi ya dunia ya ‘Guinness World Records’ kwa kuwa mwanamke mwenye kucha ndefu zaidi ameeleza kuwa anapitia changamoto nyingi kutokana na kucha hizo.

Kwa mujibu wa tovuti ya #DailyStar Diana anasema anapata tabu sana anapo kwenda chooni, kuvaa nguo na imefikia mahali hata kuendesha gari hawezi tena.

Mwanamke huyu raia wa kutoka nchini Marekani ambaye ana umri wa miaka 64, hajawahi kukata kucha zake tangu mwaka 1997 na hadi sasa zina urefu wa futi 42.

“Kila kucha moja huchukuwa hadi masaa 10 kuisafisha tu, mara ya mwisho kuzipaka rangi ilikua wiki iliyopita na nilitumia siku nne" alisema Diana

Aidha ameweka wazi kuwa kucha hizo zina kumbukumbu ya mtoto wake wakike aliyefariki akiwa na miaka 16, na siku moja kabla ya kufariki alikuwa akiziosha na kuzisafisha kucha hizo, hivyo anaona akizikata ni kama ameondoa kumbukumbu ya mtoto wake.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags