Amuua aliemzidi mwanae darasani, India

Amuua aliemzidi mwanae darasani, India

Jamani jamani sio powa kila siku mambo ya ajabu yanazidi kuibuka, Mvulana mmoja mwenye umri wa miaka 13 amefariki baada ya kulishwa sumu na Mama wa Mwanafunzi mwenzake baada ya kumshinda katika masomo Shuleni eneo la Mji wa Pwani wa Karaikal Kusini mwa India.

Bala Manikandan ambaye alikuwa ni Mwanafunzi wa Darasa la 8, alishika nafasi ya kwanza katika masomo na shughuli za ziada Shuleni, jambo lililomkwaza Mama wa Mwanafunzi mwenzake ambaye kwa sasa amekamatwa kwa tuhuma za mauaji.

Siku ya Ijumaa, Mshukiwa aliyetambulika kwa jina la Sahayarani Victoria, alidaiwa kujifanya Mama Mzazi wa Bala na kwenda kumfuata katika mlango wa Shule hiyo na kumkabidhi Kijana huyo chupa iliyokuwa na kinywaji.

Kijana huyo alikuwa akijiandaa kutumbuiza kwenye hafla ya kitamaduni ya siku ambayo hufanyika kila mwaka katika shule hiyo na ndipo alipokunywa kinywaji hicho ambapo muda mchache akaanza kujisikia vibaya, kutapika kabla ya kufariki jumamosi usiku.

Wazazi wa Bala waliwasilisha malalamiko katika Kituo cha Polisi cha eneo hilo baada ya kanda ya CCTV kumuonesha Victoria akimwomba Mlinzi ampelekee mvulana huyo chupa hizo, Madaktari wamesema Mvulana huyo alifariki kutokana na kukosa hewa baada ya chembechembe za chakula kuingia kwenye mfumo wake wa upumuaji.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags