Amshtaki mfanyakazi mwenzake kwa kumvunja mbavu wakati anamkumbatia

Amshtaki mfanyakazi mwenzake kwa kumvunja mbavu wakati anamkumbatia

Upendo ni kitu cha bure na kuna aina mbalimbali za kuonesha upendo huo, mojawapo ni kitendo cha kukumbatiana.

Katika nchi ya China, mwanamke mmoja amemshtaki mfanyakazi mwenzake baada ya kinachodaiwa ni kuvunjwa kwa mbavu zake wakati wa kitendo hicho.
 
Mwanamke huyu anayetokea katika mji wa Yueyang amemfikisha mfanyakazi mwenzake katika mahakama ya Yunxi akiomba fidia ya fedha.

Alisema kuwa alikuwa anapiga story na mwenzake ambapo mwanaume huyo alimfuata na kumkumbatia kwa nguvu, kitendo kilichomfanya apige kelele kwa maumivu. Hata hivyo aliendelea kujisikia maumivu hata baada ya kutoka kazini na akajipaka mafuta ya moto kifuani bila kwenda kupata matibabu hospitalini.

Siku tano baada, maumivu yake yaliongezeka kupita mfano na ndipo alipoamua kwenda hospitalini. Majibu yalionesha kuwa mbavu zake tatu, mbili za upande wa kulia na moja ya kushoto zilikuwa zimevunjwa.

 
Ilimlazimu kupumzika kwenda kazini na hivyo kupungukiwa kwa kipata chake, huku bili za matibabu za hospitali zikizidi kuongezeka.

Baada ya mizengwe yote, alijaribu kumtafuta mfanyakazi mwezake huyo ambaye aligoma kabisa kumpa usaidizi wowote ule na hivyo kuamua kumpeleka mahakamani akidai fidia ya yuan 10,000 sawa na sh3,439,000.
 
Kuweni makini na hugs zenu jamani..






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Detricia Pamba

A Digital Journalist, Content Creation Executive at Mwananchi Communications Ltd and Chief Editor of Mwananchi Scoop. I'm also writes stories around Technology, every Wednesday on Mwananchi Scoop. My other famous segments on Mwananchi Scoop include LISTI and WHO’S HOT.


Latest Post

Latest Tags