Amshtaki baba yake kwa kumlazimisha kuolewa na mwanaume asiyemjua

Amshtaki baba yake kwa kumlazimisha kuolewa na mwanaume asiyemjua

Binti mmoja aliefahamika kwa jina la Fatima Aliyu mwenye umri wa miaka 20 kutoka Kaskazini mwa Nigeria amemshtaki baba yake kwa kumlazimisha kuolewa na mtu asiyemfahamu, ripoti ya vyombo vya habari nchini humo imeeleza.

Wakili wa binti huyo aliiambia mahakama ya Sharia (ya Kiislamu) katika jimbo la Kaduna kwamba tayari alikuwa na mtu anayempenda. Alisema kuwa mwanamke huyo hakuwa akimshtaki baba huyo kwa kutomheshimu.

Kwa upande wa baba huyo aliambia mahakama kuwa marehemu wazazi wake walimchagulia bintiye mume walipokuwa hai na alitaka kuheshimu matakwa ya wazazi wake ambao ni bibi na babu wa binti yake.

Jaji Malam Aiyeku Abdulrahman aliamua kuwa ingawa baba ana haki ya kumchagulia bintiye mume, ndoa ya kulazimishwa haikuhimizwa.

Aidha alimshauri mwanaume huyo kuwa mvumilivu kwa bintiye. "Mruhusu amlete mtu ambaye anataka kufunga nae ndoa ikiwa umefurahishwa na dini na tabia yake, unamruhusu kuolewa," hakimu alisema

 
Chanzo BBC






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags