Amsaidia mwanamke kujifungua wakiwa kwenye ndege

Amsaidia mwanamke kujifungua wakiwa kwenye ndege

Mwanaume mmoja aitwaye Hassan Khan (28) aliyekuwa safarini akitokea mapumziko ambaye pia ni Daktari ameingia kwenye vichwa vya habari katika televisheni mbalimbali baada ya kumsaidia mwanamke mjamzito kujifungua wakati ndege ikiwa angani.

Kufuatiwa na ripoti za vyombo vya habari mbalimbali vilieleza kuwa ndege hiyo ilikuwa ikitokea Amman Jordan na kuelekea London ilishakuwa angani kwa masaa mawili, ambapo baada ya wahudumu kuona hali inakuwa mbaya kwa mwanamama huyo waliamua kuuliza abiria iwapo kama kuna daktari ndipo Hassan kujitokeza kumsaidia mwanamke huyo.

Kutokana na tukio hilo kutokea ghafla marubani wa Shirika la ndege la Wizz waliamua kubadili njia na kuelekea uwanja wa ndege ulioko jirani kwa ajili ya kumfikisha hospitali mwanamke huyo, aidha taarifa zilizotolewa baadae zilieleza kuwa mama na mtoto wake wa kike wote wapo salama.

Hii si mara ya kwanza kwa mjamzito kujifungua katika anga, Mwezi Mei mwaka jana, Abigail Amorett (17) alipata uchungu wakati wa safari ya ndege kutoka Managua, akielekea Miami.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags