Ampiga mbunge mwenzake wakati bunge likiwa live

Ampiga mbunge mwenzake wakati bunge likiwa live

Vurugu zilizuka katika bunge la Senegal siku ya Alhamisi baada ya mbunge mwanamume kumpiga mwenzake wa kike kichwani wakati wa bunge. Tukio ambalo lilionyeshwa moja kwa moja (live) kwenye televisheni.

Ilikua ni wakati wa uwasilishaji wa bajeti, ambapo kuna maneno yalitamkwa na kupelekea mbunge wa upinzani Massata Samb kuondoka jukwaani na kuelekea kwa Amy Ndiaye Gniby wa muungano tawala wa Benno Bokk Yakaar na kumpiga kichwani.

Aidha katika kulipiza kisasi, Bi Gniby alimrushia kiti Bw Samb, kabla ya wabunge wengine kuingilia kati, hata hivyo machafuko hayo hayakukoma huku wabunge hao wakibadilishana mapigo na kusababisha kusitishwa kwa kikao hicho.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags