Amouta kuchukua mikoba ya Nabi AS FAR Rabat

Amouta kuchukua mikoba ya Nabi AS FAR Rabat

‘Klabu’ ya AS FAR Rabat ya Morocco imefikia makubaliano ya kumteua mkufunzi, Hussein Amouta kuwa ‘kocha’ mkuu klabuni hapo kwa ajili ya kuchukua mikoba ya Nasreddine Nabi anayedaiwa kwenda Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini.

Inaripotiwa kuwa Amouta mweye umri wa miaka 54 ambaye raia wa Morocco kabla ya kuteuliwa na ‘klabu’ hiyo alijiuzulu kama ‘kocha’ mkuu wa ‘timu’ ya taifa ya Jordan mwezi uliopita.

Hiyo inakuja baada ya Nabi kushindwa kuipatia taji AS FAR Rabat katika fainali ya ‘Kombe la Throne’ kufuatia na kufungwa mabao 2-1, dhidi ya wapinzani wao wakubwa Raja Casablanca siku ya Jumatatu Julai Mosi mwaka huu.

Ushindi huo umeifanya Raja inayonolewa na Kocha Mkuu, Josef Zinnbauer kuendeleza rekodi nzuri ya kutopoteza kwani katika jumla ya michezo 30 iliyocheza imeshinda 21 huku tisa iliyosalia ikimalizika kwa sare.

Hata hivyo hiyo ilikuwa ‘mechi’ ya mwisho kwa Nabi katika klabu hiyo ya Morocco kabla ya kudaiwa kuelekea Chiefs ambako huenda akatambulishwa siku zijazo.

Utakumbuka April mwaka 2021 ‘kocha’ huyo aliwahi kuiogoza klabu ya Yanga kwa mkataba wa mwaka mmoja na nusu amapo aliweza kutwaa makombe misimu miwili na kuipeleka timu hiyo nusu fainali ya kombe la shirikisho Afrika.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post