Amkata mumewe sehemu za siri na kuzitupa chooni

Amkata mumewe sehemu za siri na kuzitupa chooni

Mwanamke mmoja kutoka nchini Brazil mwenye umri wa miaka 34 ambaye hajafahamika jina amejisalimisha kwa polisi Disemba 22 na kukiri kukata sehemu za siri za mumewe na kuzitupa chooni .

Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini humo vimeeleza kuwa mwanamke huyo alikata sehemu hizo za mumewe kwa kutumia kiwembe baada ya kugundua kuwa mwanaume huyo alikuwa akimsaliti na mpwa wake mwenye umri wa miaka 15.

Hata hivyo mwanamke huyo ameshikiliwa na polisi kwa muda wa siku 30 kwa ajili ya uchunguzi kwa upande wa mumewe hali ya afya yake hadi sasa bado haijulikani inavyoendelea tangu afikishwe hospitali baada ya tukio hilo kutokea.

Aidha katika uchunguzi unaofanywa na polisi pia utaangalia madai ya mwanamke huyo ya kumtuhumu mumewe kutoka kimapenzi na mpwa wake wa miaka 15.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags