Amitabh Bachchan asimulia alivyokutana na MJ

Amitabh Bachchan asimulia alivyokutana na MJ

Mwigizaji mkongwe wa Bollywood Amitabh Bachchan amesema alitaka kuzimia baada ya kukuana kwa mara ya kwanza na marehemu Michael Jackson ‘MJ’.

Amitabh ameyasema hayo alipokuwa kwenye moja ya mahojiano yake ya hivi karibuni na ‘Kaun Banega Crorepati 16’ ambapo alieleza kuwa wakati yupo New York hotelini MJ aligonga kwenye chumba chake kwa bahati mbaya.

“Nilikua nikikaa katika hoteli moja huko New York, siku moja, nikasikia mlango wangu ukigongwa, nilipofungua nilishangaa sana kumuona Michael Jackson amesimama nje, ilibaki kidogo nizimie lakini nilijikaza. Nilimsalimia, naye akauliza kama hiki kilikuwa chumba changu nilipothibitisha, aligundua kuwa alikuwa amekosea.

“Baadaye, alipofika kwenye chumba chake, alimtuma mtu aje kuniita niende chumbani kwake, na hatimaye tulipata furasa ya kukaa chini na kuzungumza, licha ya umaarufu wake mkubwa alikuwa mnyenyekevu sana,” alisema Amitabh

Michael Jackson, maarufu kama 'Mfalme wa Pop', aliyezaliwa Agosti 29, 1958, huko Gary, Indiana, Marekani alifariki mwaka 2009 akiwa na umri wa miaka 50.

Amitabh Bachchan ameonekana katika filamu kama Andha Kanoon, Mohabbatein, Kabhi Khushi Kabhie Gham, Bhoothnath Returns na nyinginezo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags