Ally Kamwe afiwa na binti yake mdogo

Ally Kamwe afiwa na binti yake mdogo

Kutoka katika Instagram ya Afisa Habara wa klabu ya Yanga  Ally Kamwe ameandika ujumbe mzito baada ya kupokea ujumbe kuwa binti yake mdogo amefariki akiwa nchini Addis Ababa, alipokuwa anaelekea na klabu yake katika mchezo wao wa marudiano na timu ya Al hilal Sudan.

Ujumbe huo ukiwa unaeleza “Ndani ya uwanja wa Bole, pale Addis Ababa, Ethiopia.. Dakika chache kabla hatujaunga ndege kwenda Khartoum, nilipokea meseji ya kuumiza sana kwenye simu yangu.“Ali, mtoto amefariki” Binti yangu mdogo, Latiffah alikuwa ameaga dunia” ameandika Ally Kamwe

Aidha afisa habari huyo aliendelea kwa kuandika kuwa “Nilishituka sana. Mikono ikatetemeka. Mwili ukapata ganzi ya ajabu,SikuaminiNi kama mshale ulirushwa ghafla kwenye mgongo wangu. Nikaanza kusikia maumivu makali moyoni, Nikajipa ujasiri wa kupiga simu ya Mama yake.. Alipokea, Lakini hakuweza kutoa neno lolote zaidi ya kilio kilichosindikizwa na kwikwi kali” ameandika Ally Kamwe

Kwa maskitiko makubwa alimaliazia kwa kueleza kuwa “Nikapoteza ujasiri. Sikio langu lilishindwa kuendelea kumsikia Mama Latiffah akiendelea kulia. Nikakata simu na hapa ndio nikaamini kuwa Latiffah hayupo tena duniani, Ukiwa mzazi, utanielewa pindi unapopata Taarifa ya kifo cha ghafla cha mtoto ambaye uliondoka nyumbani na kumuacha salama kabisa”


“Shukrani sana kwa uongozi na kwa wachezaji wa Yanga  Haikuwa rahisi kwangu hata kidogo kuishi Sudan huku ukijua kuna sehemu ya maisha yako haipo tena. Lakini niliuvisha moyo wangu koti la ujasiri. Kila nilipohisi kushindwa, nilikimbia chumbani na kujifungia.. Nikitoa nje naendelea na kazi. Sikutaka wengine waone ni jinsi gani nimesambaratika moyoni.. Alhamdulillah Rest in Peace Tiffah. Baba Atakuona tena wakati mwingine” ameandika Ally Kamwe

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags