Aliyesafiri kwa baiskeli siku nane akataa pesa za Davido

Aliyesafiri kwa baiskeli siku nane akataa pesa za Davido

 Kijana Emmiwuks aliyepata umaarufu mkubwa baada ya kusafiri kwa siku nane kwa kutumia baiskeli ili aonane na nyota wa muziki Nigeria, Davido amekataa kutuma ‘akaunti’ namba yake ya bank ambayo mkali huyo wa muziki alimuomba ili amtumia pesa za kurudi kwao.

Emmiwuks amekataa ‘ofa’ hiyo na kudai kuwa kuonana na Davido kuna thamani kubwa kuliko pesa anazotaka kumpatia.

Kama kawaida kupitia ukurasa wake wa #Twitter kijana huyo ametoa shukurani kwa kudai kuwa anaheshimu ‘ofa’ aliyopewa na Davido lakini atasubiri hadi arudi Lagos kwani kuonana naye kuna thamani zaidi, huku akisisitiza kuwa amebeba zawadi anayotaka kumkabidhi.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags