Aliyemchoma moto Cheptegei afariki dunia

Aliyemchoma moto Cheptegei afariki dunia

Dickson Marangach Aliyekuwa mpenzi wa mwanariadha wa Olimpiki wa Uganda, Rebecca Cheptegei amefariki dunia usiku wa kuamkia leo.

Marangach alifariki dunia akiwa katika Chumba cha Wagonjwa Mahututi (ICU) kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mafunzo ya Moi (MTRH) mjini Eldoret, wakati akipatiwa matibabu ya moto wa petroli alioungua huku mwili wake ukiwa na majeraha ya zaidi asilimia 30.

Taarifa za Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), zilieleza alikuwa katika hospitali hiyo ambayo pia Cheptegei alikuwa akitibiwa kabla hajafariki dunia.

Katika tukio hilo lililohuzunisha wengi, Cheptegei alifariki dunia Septemba 5, 2024 wakati akipatiwa matibabu ya majeraha aliyoyapata baada ya kumwagiwa petroli, kisha kuchomwa moto na mpenzi wake huyo.

Kwa mujibu wa Nation ya Kenya, watu walimkuta katika hospitali hiyo ikiwa ni siku mbili tangu kuchomwa moto na Marangach, huku sababu ikitajwa ni ugomvi uliosababishwa na mgogoro kwenye uwanja na nyumba.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali hiyo, Dk Owen Menach ambaye pia ni mkurugenzi wa Huduma za Kliniki na Upasuaji, alisema mwanariadha huyo alilazwa ICU na alifariki dunia kutokana na kuwa katika hali mbaya iliyotokana na majeraha ya moto.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags