Aliyekuwa waziri mkuu wa Uingereza aangukia kwenye utangazaji

Aliyekuwa waziri mkuu wa Uingereza aangukia kwenye utangazaji

Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson ameibuka kwenye uandishi wa habari na atafanya kazi katika kituo cha televisheni cha GB News kilichopo jijini London.

Kwa mujibu wa BBC imeeleza kuwa Johnson atafanya kazi katika kituo cha habari cha GB kama mtangazaji, mtayarishaji wa vipindi na mtoa maoni huku akipewa jukumu la kufanya matangazo ya moja kwa moja ya uchaguzi ujao nchini humo.

Boris ambaye alijiuzuru Uwaziri Mkuu nchini humo mwanzoni mwa mwaka huu aliwahi kufanya kazi hiyo katika vyomba vya habari tofauti ikiwemo gazeti la The Daily Telegraph, kuwa Mhariri wa 'The Spectator' na mwandishi wa Brussels.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags