Aliyehusishwa kubeba dawa za kulevya za Diddy akutwa na hatia

Aliyehusishwa kubeba dawa za kulevya za Diddy akutwa na hatia

Kijana moja aliyedaiwa kuwa ndiyo mbebaji wa dawa za kulevya za #Diddy, #BrendanPaul ameshitakiwa jana Jumatano kwa kosa la kukutwa na dawa aina Cocaine baada ya kukamatwa mwezi uliopita.

Kwa mujibu wa Tmz News imeeleza kuwa Paul alikuwa karibu na Diddy, alikuwa anajua mambo mengi ya rapa huyo ikiwemo mambo yake machafu ya uhalifu na unyanyasaji wa kingono kwa wanawake.

Hata hivyo imeripotiwa kuwa shitaka lake jingine la kukutwa na kete za bangi limetupiliwa mbali kulingana na hati ya mahakama baada ya wakili wake kudai kuwa kosa hilo ni fupi sana hivyo watalishugulikia katika chumba cha mahakamani

Ikumbukwe kuwa Paul ambaye aliwahi kuwa mchezaji wa mpira wa kikapu alikamatwa mwezi Machi katika uwanja wa Ndege wa Miami-Opa Locka baada ya wafadhili kupekua begi lake na kudaiwa kupata Cocaine na kete za bangi.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags