Alikiba akanusha kufanya kolabo na Davido

Alikiba akanusha kufanya kolabo na Davido

Baada ya kusambaa kwa List ya ngoma  kutoka kwenye albam mpya ya star kutoka nchini Nigeria Davido ikiwa inaonesha jina la Staa wa muziki kutoka Nchini Alikiba likiwa kama moja wapo la Mastaa walioshirikishwa katika Album hiyo ambayo inadaiwa kutengenezwa na watu ambao sio Rasmi.

Kupitia Mahojiano yake na moja ya chombo cha habari nchini mwanamuziki huyo amekanusha taarifa hizo kwa kusema hajakutana nazo huku akisema kuwa hamna kolabo kati yake na msanii huyo

"Sijakutana na Tracklist hiyo mpaka sasa na hamna Kolabo ya Alikiba na Davido" amesema King Kiba

Mbali na hivyo alifunguka kuhusu mashabiki kuzungumza kuwa ameacha muziki na kutimkia katika kilimo, ameelezea na kusema kuwa licha ya kuwa kwenye Kilimo lakini ataendelea kufanya kazi za muziki kama kawaida.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post