Alichosema Soggy baada ya Mahakama kuamuru walipwe Sh700 Milioni

Alichosema Soggy baada ya Mahakama kuamuru walipwe Sh700 Milioni

Na Glorian sulle

Baada ya Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar Es Salaam, kuamuru Anselm Tryphone Ngaiza (Soggy Doggy) na Florence Kasela (Dataz) kulipwa pesa zaidi ya Sh700 milioni baada ya kushinda kesi ya madai ya hatimiliki ya wimbo wao 'Sikutaki', Soggy ameieleza Mwananchi namna walivyogundua kuwa wimbo wao umetumika.

Katika hukumu hiyo iliyotolea jana Julai 26, 2024 dhidi ya Kampuni ya Home Box Office (HBO) ya Marekani, chini ya mawakili wa Kampuni ya Markel Advocats Soggy amesema waligundua wimbo wao huo umetumika katika Filamu ya 'Sometimes in April’ iliyochezwa na staa Idris Elba baada ya miaka kumi kupita tangu kutoka kwake mwaka 2005, na baada ya kujiridhisha alianza kutafuta mawakili kujua haki yake katika filamu hiyo.

“Wimbo wetu huu ulitoka mwaka 2004 na kutumika katika filamu hiyo mwaka 2005, baada ya kugundua hilo kupitia marafiki zangu ndipo 2015 tulianza kutafuta mawakili,” amesema Soggy Doggy.

Soggy Doggy amesema baada ya kuona gharama za kulipa mawaakili ni kubwa ndipo walianza kujichanga na mwaka 2017 walipata mawakili wa kuanza kuichambua kesi hiyo kisha wakawatumia e-mail wahusika wa filamu hiyo.

“Baada ya kujibiwa e-mail na kumaliza vyote tulivyoelekezwa tulipewa utaratibu ambao uliwahusisha COSOTA, mpaka kufika mahakamani ilikuwa 2021 tukafungua kesi rasmi,” amesema.

Soggy Doggy amesema kwa taratibu za kimahakama, Home Box Office wamepewa mwezi mmoja wa kukata rufaa, baada ya muda huo kupita wasipofanya hivyo utaratibu wa kulipwa utaanzia hapo.

Kwa mujibu wa Soggy Doggy, wimbo huo yeye ndiye aliuandika, kisha ukaja kuimbwa na Dataz aliyeshirikiana naye.

Soggy Doggy aliyewahi kutamba miaka ya 2000 kwa umahiri wake katika utunzi wa nyimbo zenye ujumbe kama vile Kibanda cha Simu na Fagilia, kwa sasa amejikita katika tasnia ya habari kama mtangazaji wa Mjini FM.criptions






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post

Latest Tags