Al-Hilal yaitaka saini ya winga wa Man United

Al-Hilal yaitaka saini ya winga wa Man United

‘Klabu’ ya Al-Hilal ipo kwenye mipango ya kumnunua winga wa klabu ya #ManchesterUnited, raia wa Argentina #AlejandroGarnacho, ambaye kwa sasa yupo katika mashindano ya Copa America.

Kwa mujibu wa The Sky Sport imeeleza kuwa ofa ya kumuhitaji mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 19 inaweza kutumwa wakati wowote.

Taarifa zinasema winga huyo anaweza kufikiria kuhama kwa sababu yuko kwenye mkataba wa kawaida ikilinganishwa na baadhi ya wachezaji wanaolipwa fedha nyingi ‘klabuni’ hapo.

Hata hivyo, kumshawishi kinda huyo kuachana na Ligi ya Uingereza na ‘soka’ la Ulaya kwa ujumla katika umri huo mdogo kunaweza kuwa jambo lenye changamoto kwa Man United.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags