Akothee akataa kushirikishwa vita aliyoanzisha Khaligraph

Akothee akataa kushirikishwa vita aliyoanzisha Khaligraph

Mwanamuziki kutoka #Kenya, #Akothee, awakataa wakenya wenzake waache kum-tag kwenye kauli zao za kudhihaki muziki wa Tanzania.

Akothee amekataa kuingilia vita hiyo ya kumuziki ambayo ilianzishwa hivi karibuni na msanii wa hip-hop Kaligraph kutoka nchini humo

Mwanadada huyo ame-share video akiwa anaongea kwa msisitizo kuwa yeye hawezi kuingilia vita ambayo haimuhusu na kusema kuwa mashabiki wake wengi wanatokea Tanzania kwa sababu ndiyo watu wanaopenda nyimbo zake na sio wakenya wenzake na wengine ni marafiki zake.

Aliendelea kusema kuwa mashabiki kutoka Kenya waliwahi kumwambia kuwa haimbi, hana mashabiki Kenya, hivyo basi  hawezi kugombana na majirani zake.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags