Akataa kutumbuiza kwenye uapisho wa rais Tinubu

Akataa kutumbuiza kwenye uapisho wa rais Tinubu

Mwimbaji kutoka nchini Nigeria, Tochukwu Ojogwu maarufu kama Odumodublvck amekataa mwaliko wa kutumbuiza kwenye shughuli ya uapisho wa Rais mteule wa Taifa hilo, Bola Ahmed Tinubu mwenye umri wa miaka 71.

Odumodublvck amesema walijaribu kumtafuta ili akatumbuize kwenye uapisho wa rais huyo kitendo ambacho ana amini, hawakufanya utafiti vizuri dhidi yake, hatua hiyo imetafsiriwa kama mkali huyo wa "Where dem dey?" kwamba hataki kumuunga mkono Tinubu kama Rais wa Nigeria.



Ikumbukwe tuu Tinubu anatarajiwa kuapishwa siku ya Jumatatu, Mei 29, mwaka huu baada ya kuchaguliwa mwezi Februari, ambapo alishinda uchaguzi huo uliokuwa na mzozo kwa asilimia 36.61 ya kura, jumla ya kura 8,794,726.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags