Ajifanya mwanaume ili apate nafasi ya kuchimba madini

Ajifanya mwanaume ili apate nafasi ya kuchimba madini

Duh! Ama kweli mambo ni mengi muda mchache, ukiambiwa kuwa uyaone si maghorofa, basi bwana leo katika segment yetu ya unique story tumekusogezea mwanamama ambaye ameamua kujibadilisha mwonekano wake kuwa kama mwanaume ili apate nafasi ya kuchimba madini.

Pili Hussein baada ya kuolewa hakufurahia ndoa yake kwani mume wake alikuwa mkorofi na mnyanyasaji sana, alipofikisha umri wa miaka 31 aliachana na mume wake akaamua kwenda Mererani kutafuta maisha, alipofika mgodini alianza upelelezi wa chini chini akaambiwa kwamba wanawake hawaruhusiwi kuchimba madini na hata wanaolazimisha kuchimba wanaonewa sana.

Ndipo mwanamama huyo akapata wazo la kujifanya mwanaume, akaanza kuvaa kama wanaume, akabadili jina na kujiita 'Uncle Hussein'.

Tangu mwaka 1987 mpaka 2015 alifanya kazi na wanaume lakini hawakuwahi kumshtukia kwamba ni mwanamke, kuna muda ilimbidi aanze kunywa pombe za kiume ilimradi tu aendane na wanaume, ingawa anasema alikuwa hamezi pombe alikuwa anatema lakini wenzake walijua ni mlevi mwenzao.



Miaka ya 1990 alifanikiwa kupata mawe mawili ya tanzanite, moja la gram 1,000 na jingine la gram 800, hapo maisha yake yalianza kubadilika maana alinunua vifaa bora zaidi vya uchimbaji

Mpaka sasa mwanamama huyo ni bosi ana kampuni ya uchimbaji madini, ameajiri zaidi ya watu 70, anamiliki ardhi ekari 150, mifugo na kadhalika.

Ndoto kubwa ya Pili ni kufundisha mabinti uchimbaji na biashara ya madini, pia anatamani kuona jamii ikibadilika kimtazamo na kuchukulia kawaida wanawake wanaochimba madini kujitafutia maisha.

Pili aligundulika ni mwanamke baada ya kutokea tukio la ubakaji na yeye akituhumiwa kufanya ubakaji huo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags