Aiba nguo za ndani za wanawake ili kumzawadia mpenzi wake

Aiba nguo za ndani za wanawake ili kumzawadia mpenzi wake

Kijana mmoja kutoka nchini Kenya mwenye umri wa miaka 19, aliefahamika kwa jina la Joel Kimurgor anadaiwa kuiba nguo za ndani za wanawake katika kijiji cha Tegeyat kaunti ya Nand chini humo.

Kwa wiki kadhaa kumekuwa na visa vya wanawake kurepoti upotevu wa nguo za ndani kutoka kwenye kamba nyakati za usiku, ambapo wakazi wa eneo hilo walianzisha zoezi la upekuzi kutoka nyumba moja hadi nyingine.

Kulingana na msako huo jana Jumatatu mtuhumiwa alikamatwa akiwa na nguo 20 za ndani za wanawake ambapo zilikutwa zikiwa zimefungwa kwenye mifuko nyumbani kwake.

Joel amekiri kuiba nguo hizi kutoka katika nyumba tofauti tofauti mtaani hapo ili kumfurahisha mpenzi wake ambae alimwomba amnunulie nguo mpya za ndani kama njia ya kumuonesha mapenzi.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags