Ahmed Ally: Tumeisaidia Serikali kutangaza vivutio

Ahmed Ally: Tumeisaidia Serikali kutangaza vivutio

Kutoka kwenye ukurasa wa Instagram wa Anaandika wa Ahmed Ally             ameandika ujumbe huu hapa bwana

''Bodi ya Utaliii ya Afrika Kusini imeilipa klabu ya Tottenham ya England Euro Milioni 42.5 (Zaidi ya Tsh Bilioni 106) ili kutangaza Utalii wa Afrika kusini kwa kipindi cha miaka mitatu

Baadhi ya Wananchi wa Afrika kusini wamekosoa deal hilo wakisema hizo fedha ni nyingi ambazo zingeweza kutatua changamoto nyingine.

Kwa kufahamu umuhimu wa Utalii, Simba tumeamua kuisaidia Serikali kwenye kutangaza vivutio vya Tanzania.

Hapa tumeisaidia Serikali kuokoa mamilioni ya fedha ambayo yangetumika kwenye matangazo

Japo bado tunahitaji kujitangaza zaidi hasa katika platform za kimataifa lakini tayari Simba tumeipunguzia gharama Nchi yetu

Fedha ambazo zingetumika kulipa Matangazo ya sasa zitaelekezwa kwenye miradi mengine ya maendeleo.

VISIT Tanzania 🇹🇿 Home of Simba

Ebwanaa unaunga mkono hoja ya Ahmed Ally kwa asilimia ngapi?dondosha comment yako hapo chini.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags