Ahmed Ally: October 1 ni siku ya hukumu

Ahmed Ally: October 1 ni siku ya hukumu

AHMED ALLY: OCTOBA SIKU YA HUKUMU
Semaji la Simba Ahmed Ally naye hajakaa kinyonge baada ya kutoka sare katika mchezo wao na Power Dynamos uliochezwa nchini Zambia, ameunguruma kupitia Instagram yake na kueleza kuwa hicho walichokipata kina manufaa.

Kupitia Instagram yake ameandika, “Sare yenye manufaa kwetu , ingawa tungeweza kupata ushindi mkubwa zaidi kama tungetumia kila nafasi tuliyoipata lakini huo ndiyo mpira.

Asante Power Dynamos kwa kutupa mchezo mzuri wenye hadhi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Karibuni Dar es Salaam tuje tumalizane.

Leo ilikuwa ni siku ya kusoma mashtaka, Oktoba 1 ni siku ya hukumu”.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post